Bukavu : Wakaazi walaumu msongamano kutokana na vifaa vya ujenzi pamoja na gari barabarani

Mji wa Bukavu

Msongamano waripotiwa kwa mara kwa mara kwenyi eneo SINELAC mbele ya kituo cha afya Saint Luc pa Nyawera mjini Bukavu. Vyombo vya ujenzi vikifunga barabara na hata nafasi ya wapita njia. Hali ambayo husababisha ajali za barabarani.

Malalamiko ya raia walio wengi wapitao nafasi hiyo ya mtaa wa Ibanda mjini Bukavu.

« Je viongozi wa mji waweza kutusaidia kuondowa vyombo hivyo vinavyozuia watu kupita na kwenda kwenyi shuguli mbali mbali. Hali inayosababishwa na watu wenyi nia mbaya « moja wa watumiaji nafasi hiyo anena kwa la ronde info.

Raia waomba kwa viongozi wa mji mafasirio kamili kuhusu vyombo vya ujenzi na gari vyenyi kufunga barabara karibu eneo zote mjini Bukavu. Wakiomba pia viongozi kuwa na zamiri safi kwani hawa wajitahidi kusafisha barabara viongozi watakapofika mjini Bukavu toka Kinshasa na baada ya hapo wapachika mikono.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire