Balozi Mike Hammer afahamisha utashi wa kusaidia mpango wa mwaka wa shauri la vijana jimboni Kivu ya kusini na kusherekea kwenyi kikao kuhusu mpango huo mwezi aprili ujao.
Hayo ni matamshi ya balozi Mike Hammer kwa ujumbe wa shauri la vijana Kivu ya kusini.
Huyu anena kufuravishwa mpango wa mwaka wa shauri la vijana Kivu ya kusini, alihakikisha kwamba atafanya yote iwezekanayo ili vijana hawa wapate msaada toka shirika la kimataifa USAID.
Wakati huo Prezidenti wa shauri la vijana Kivu ya kusini Joella Sambo aomba kubadili ujuzi kati ya vijana wa DRC na wa Marekani ili kuinua mazao ya kazi kwenyi soko nchini DRC.
Balozi huyo aliwaambia vijana hawo kwamba ujenzi wa Marekani ni hatua pamoja na maoni ya vijana wa nchi hiyo. Prezidenti wa shauri la vijana Kivu ya kusini anena kufuravishwa kwa mapokezi bora ya balozi kuhusu swala la vijana wa DRC kwa jumla na Kivu ya kusini kwa pekee.
Akiamini kwamba ahadi yake balozi wa Marekani itarahisisha vijana wa DRC kuwa na umoja duniani ili kuijenga ulimwengu iliyo bora, akitoa mfano wa Marekani nchi yenyi samani kubwa kiutu ni kidemokrasia ulimwenguni.
Chumba cha wandishi
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.