Rutshuru : Wakaazi wa Nyamilima waomba viongozi usalama kutokana na mauaji eneo hilo

Walimaji wawili wa Nyamilima wilayani Rutshuru waliuliwa ijumaa iliyopita na wanaozaniwa wana mugambo FDLR wenyi kupatikana pa Nyamatwitwi umbali wa kilomita kumi na Nyamilima.

Duru toka huko zanena kwamba mauaji hayo yatokana na mizozo kati ya jirani wa shamba za watu hawa , ambaye alishawishi wa FDLR kuondolea maisha wahanga.

Upande mwengine ni kwamba hawa hawakulipa ushuru unaolazimishwa na wanamugambo FDLR kwa kila mwanainchi. Ushuru ambao ni franka 5000 hadi 50000 franka za kongo kwa kila shamba na kwa kila mavuno.

Mtetezi wa haki za wana Rutshuru Aimé MUKANDA MBUSA afahamisha kwamba mwili moja kati ya miwili mbili ulipatikana na kuzikwa juma mosi hapo jana. Mwili mwengine bado kugundiliwa.

 » Tunaomba viongozi kuzi gonga ma kundi hizo zenyi kushikilia silaha pa Binza na kwenyi eneo lote la Rutshuru anena » mtetezi wa haki za wana Rutshuru

Tufahamishe kwamba ni watu 11 wakiwa walimaji ndio wameuliwa pa Nyamilima na Buramba tangu mwezi juni 2021.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire