Nyiragongo : Vijana wa Kiziba 2 waomba serkali kuwalindia usalama eneo hilo la jimbo la Kivu ya kaskazini

Prezidenti wa vijana pa Kiziba ya pili eneo la Mudja wilayani Nyiragongo Akilimali Mulindwa Adelard.

Akihojiwa na mwana ripota wa la ronde info hii juma tano tarehe 23 februari , Prezidenti wa vijana pa Kiziba ya pili eneo la Mudja wilayani Nyiragongo Akilimali Mulindwa Adelard alaumu kutojihusisha kinaganaga kwa serkali ili kuazibu visa vya ujambazi nafasi hiyo.

Kisa cha hapa karibuni ni mtoto moja mwenyi umri wa miaka kumi na miwili aliyeuliwa akitoka shuleni, kwa kupigwa jiwe kichwani, na mlevi moja kati ya wawili waliokuwa wakigombana kwenyi kilabu cha pombe za kulevya .

Adelard Mulindwa anena kwamba baada kumjeruhi mtoto, alipelekwa hima kunako kituo cha afya ambako aliaga dunia.

Kiongozi wa vijana pa Kiziba ya pili anena kushangaa kuona mhusika na kitendo cha kifo haijulikane mahali alipo baada ya mazishi kufanyika tarehe 19 februari. Na kwamba hakuna uchunguzi kamili uliofanyika ili mhusika afunguliwe kesi na kuazibiwa kulingana na sheria.

Vijana wa Kiziba ya pili washangaa pia kuona mwenyeji kilabu cha pombe za kulevya abaki pia bila serkali kuchukuwa hatua kuhusu vinywaji hivyo vya kulevya ambavyo ni chanzo cha mazara eneo hilo.

Juvénal Murhula.

1 Comment

Poster un Commentaire