Goma: Mwanabunge wa taifa Josué Mufula tayari ameondowa mashtaka dhidi ya shirika Premidis baada ya uchunguzi.

Mwanabunge wa taifa Josué Mufula akitembelea shirika Premidis

Baada ya uchunguzi kwa makini, mwanabunge wa taifa mchaguliwa wa Goma Josué Mufula aangazia kwamba yaonekana. ni wanasiasa wenyi nia mbaya pamoja na viongozi wa kijeshi kadhaa ndio chanzo cha pombe za kulevya ambazo zaharibu maisha ya vijana jimboni Kivu ya kaskazini. Kinyume na shirika Premidis ambalo lahusika zaidi na kazi za maendeleo jimboni humo.

Alinena hayo hii ijumaa tarehe 23 februari baada ya kukutana na viongozi kadhaa wa shirika Premidis mjini Goma, akitokea mjini Kinshasa.

Mwanabunge Josué Mufula alijionea binafsi kwamba pombe za kulevya hazihusu shirika Premidis bali wanasiasa wenyi nia mbaya pamoja na viongozi wa kijeshi ambao waendesha kazi hizi za kimagendo saa za usiku .

Josué Mufula aahidi kukutana na waziri husika na biashara ya nje nchini wakati wa kikao bungeni, ili atowe mafasirio kamili kuhusu kuingizwa kwa biashara haramu jimboni Kivu ya kaskazini.

 » Kwa sasa waziri atafasiria pamoja na mkurugenzi wa shirika la uchunguzi OCC namna gani vyafikishwa vinywaji vyenyi kuondowa maisha ya vijana jimboni Kivu ya kaskazini, » asisitiza mwanabunge huyo.

Josué Mufula aunga mkono miradi kadhaa inayotekelezwa na shirika Premidis yaani ujenzi wa shule , barabara n’a kadhalika. Akifahamisha kwamba shirika Premidis latumika kisheria nchini DRC . Akiongeza kwamba shida ni kwamba shirika Premidis halifanye mawasiliano bora.

Shirika Premidis lafanya pia kazi za kutengeneza mafuta na hata sabuni.

Upande wa shirika Premidis Bwana Zebedée husika na maswala ya wafanya kazi aeleza kwamba njama zaandaliwa dhidi ya shirika Premidis, ila ashukuru kuona mwanabunge Josué Mufula amejionea kuwa shutuma dhidi ya shirika hilo si halali.

Kiongozi husika na swala la wafanya kazi kwenyi shirika Premidis Bwana Zebedée

 » Tunafurahi kwa shauri lake Mwanabunge Josué Mufula kuhusu kutowasiliana, na hivi tutarekebisha. Sisi tutaendelea kutumika kazi hata kama watu wataendelea kuchochea, » alihitimisha kiongozi husika na wafanya kazi Zebedée.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire