Bukavu : Raia wa kata Nkafu watolewa mingazi iliyojengwa na mtaa wa Kadutu kupitia bajeti ya pamoja

Ilifanyika hii juma mosi tarehe 26 februari 2022 sherehe za kukabizi rasmi mingazi inayojengwa kupitia bajeti ya pamoja ndani ya kata Nkafu mtaani Kadutu.

Mingazi yenyi urefu wa mita 980 , upana wa mita 2 itarahisisha watu kupita tangu kiingilio ya hospitali ya Yunivasti hadi kwenyi shule la msinji Kataliko.

Bwana Hypocrate Marume msimazi wa bajeti ya pamoja mjini Bukavu aliyetowa habari, anena kwamba mradi huo ulisapotiwa na mtaa wa Kadutu ukisaidiwa na watu wenyi moyo mwema.

« Shukrani zetu ziendee raia ya mahali yaani hôpital général, Daktari David Nanga, Mwanabunge jimboni Kivu ya kusini Nestor Balyana pamoja na Rigobert Bamba. Shukrani zetu zimuendee pia Kiongozi wa mtaa wa Kadutu Profesa Munyabene Nyembo kwa kujihusisha na kazi ya bajeti za pamoja. Tukimukumbusha kuwa kazi ni chungu tele ndani ya kata nyingine « , anena Hypocrate Marume msimazi wa bajeti ya pamoja mjini Bukavu.

Akishukuru pia shirika la raia n’a kamati ya mahali husika na maendeleo kwa kusindikiza na hata kushiriki kwenyi mwanzo wa kazi hadi mwisho. Pamoja kuhusu maendeleo ya mji wa Bukavu.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire