Chama cha kisiasa Ensemble pour la République kitag asombea uchuguzi mwaka 2023

Mwanabunge jimboni Kivu ya kaskazini Promesse Matofali afahamisha kwamba chama Ensemble pour la République chake Moïse Katumbi kiko tayari kugombea uchuguzi mwaka 2023 hapa karibuni.

Alifahamisha hii ijumaa tarehe 23 februari kwenyi uwanja wa ndege pa Goma toka mjini Lubumbashi. Akiongeza kwamba ziara yao ilikuwa na lengo la kubadili fikra kuhusu maelekezo mapya ya chama naye Prezidenti Moïse Katumbi pamoja na kuzinduwa jumba ambayo ni makao ya chama mjini Lubumbashi.

Kuhusu usalama mdogo, Promesse Matofali alaumu vikali vitendo vya kinyama wanavyo tendewa raia kote jimboni. Akiomba vyombo vya usalama kufanya kazi vilivyo ili kutekeleza amani jimboni Kivu ya kaskazini.

Promesse Mafofali ahakikisha kwamba chama chake ni tayari kwenyi uchaguzi ujao kwa ngazi zote nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Swala kuhusu msako usiohitimishwa jimboni Kivu ya kaskazini, Mwanabunge huyu anena huenda ni kutokana na uongozi wa kijeshi humu jimboni, ila inabidi msako ukomeshwe maana siyo mbinu mhimu ili kukomesha usalama mdogo jimboni Kivu ya kaskazini.

Juvénal Murhula

.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire