Goma: Mwakilishi wa SVK yaani soutien à Vital Kamerhe kwa kimombo yuko ziarani mashariki mwa DRC ili kusisimuwa kazi mbele ya uchaguzi mwaka 2023

Mratibu nchini wa Muungano SVK awasili mjini Goma hii juma pili tarehe 27 machi 2022 katika lengo la kusisimuwa kazi jimboni Kivu ya kaskazini, tukizungumza kuhusu uchaguzi na kutowa salamu zake Vital Kamerhe Prezidenti wa chama UNC kwa raia wa jimboni.

Alinena hayo baada ya kuwasili kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma hii juma pili tarehe 27 februari 2022.

Tunakuja shimika kamati ya uratubu mjini Goma na wilayani Nyiragongo. Tutaweza zunguka hapa na pale ili kuhimiza wafwasi wa chama kuhusu uchaguzi hapa karibuni. Inabidi kutumika ili kubuga ushindi kwenyi uchaguzi ujao, tukiwa na viti vingi kwenyi bunge la jimbo na hata la taifa.

Mjumbe wake Prezidenti Vital Kamerhe alifahamisha kwamba Vital Kamerhe mwenyewe apatikana kwa matunzo huko Ulaya. Akihakikisha kwamba Ana afia njema na kwamba atarudi punde si punde.

Baada ya kuwasili akijielekeza mjini Goma ambako aliweza kutanana na wafwasi wa chama ajili ya ripoti mbali mbali. Pamoja kupanga kazi za chama.

Mjumbe wa chama UNC aliahidi kutembea eneo zingine huku mashariki mwa DRC ili ya kujionea binafsi jisi zaendelea kazi za chama ajili ya kujuwa nini ifanyike ili kuboresha kazi.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire