DRC/ Yunivasti: Muungano wa ma Profesa wasitisha mgomo baada ya mazungumzo na serkali

Waziri mkuu Jean Michel Sama Lukonde wa DRC.

Muungano wa ma Profesa wa Yunivasti nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo umekubali kusitisha mgomo juma nne tarehe mosi machi baada ya kazi za uchunguzi alizoongoza waziri mkuu Jean Michel Sama Lukonde akisindikwa na waziri husika na elimu ya juu Muhindo Nzangi Butondo.

Katika tangazo lao, Profesa Rodolphe Iyolo afahamisha kwamba ni baada ya mkutano wa uchunguzi kati ya waziri mkuu akisindikwa naye husika na elimu pamoja na Muungano wa ma Profesa ndipo walifikia makubaliano.

Mwana elimu huyu aonyesha kwamba ni kutokana na utashi mwema wa serkali kutaka kujibu kwa madai ya ma Profesa, ndipo waliamuwa kusitiza mgomo.

Habari toka chumba cha mawasiliano cha Muungano wa ma Profesa zanena kwamba timu zimeundwa ili kuweka nukta kwa tangazo ambalo litasainiwa hii tarehe 2 machi 2022.

Muhindo Nzangi Butondo waziri wa elimu ya juu wa DRC

Kwa ukumbusho ni tangu tarehe 5: januari 2022, wakati wa kurudi shuleni kwa wanachuo, ndipo mgomo wa ma Profesa pamoja na walimu wasaidizi na hata wafanya kazi kwa jumla wa sekta hiyo walianza mgomo. Majadiliano yalianza hatua kwa hatua, na kufikia kusahini makubaliano na walimu wasaidizi, walimu wa ngazi za kufwata, wafanya kazi kwa jumla na baadae ma Profesa.

Duru zaongeza kwamba kazi za pamoja zaendeshwa ili kutowa maelekezo kuhusu hatua zitakazo chukuliwa kwa pande husika yaani serkali na walimu.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire