Rutshuru : Raia wakosa makao pa Buramba nyumba zikichomwa moto na wevi wenyi kushikilia silaha

Watu wenyi kumiliki silaha walishambulia Kijiji Buramba wilayani Rutshuru jimboni Kivu ya kaskazini.Duru toka huko zanena kwamba watenda maovu hawo walichoma moto nyumba takriban kumi na kupora vitu vyenyi samani kubwa.

Hayo yalifanyika usiku wa juma nne kuamkia juma tano tarehe 2 machi mwaka tunao .

Wenzetu wandishi toka Rutshuru waeleza kwamba wahanga wa ajali hiyo ya moto wabaki nje kwa kukosa makao, na kwamba hakujakuwa juhudi yoyote upande serkali ili kuwahudumia.

Hawa waomba serkali na hata mtu wa moyo mwema kuwahudumia katika hali mbovu waishi ndani baada ya ajali. Pamoja na hayo, serkali kujitahidi kwa kulindia raia usalama kwani ni kila leo ndipo shambulizi zaripotiwa. Na hayo husababisha maafa mengi.

Steward Cuma.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire