Idara ya afya jimboni Kivu ya kaskazini yatoa ripoti kamili kuhusu hali ya virusi vya korona tangu mwanzoni mwa janga.
Kutokana na jarida lake nambari 706 ya kamati husika na kupiganisha janga hilo nchini DRC ya tarehe 27 februari 2022. Tangu kutangazwa kwa virusi hivyo tarehe 10 machi 2020, visa kwa jumla ni 86.154 vilivyo hakikishwa, miongoni visa 86.152 na visa 2 vyenyi kuzaniwa.
Ripoti yaendelea kuangazia kwamba kwa jumla ni visa 62.551 ya watu waliopona, 1.335 ya watu walioaga dunia.
Upande mwengine Idara hiyo ya afya jimboni, tawi la Butembo yajulisha kwamba ni wiki mbili sasa bila kuorozesha kisa cha virusi vya korona mjini Butembo.
Jambo lafurahisha mwanabunge mchaguliwa wa Butembo Tembos Yotama, ambaye ashukuru raia kwa mcango wao. Akiomba serkali kuweka mkazo kuhusu kuingia kwa watu jimboni wakitoka nje . Namna ya kuepuka kutapanya maradhi ya korana.
Tukumbushe kwamba vipimo kuhusu virusi vya korona ni bure, ila wasafiri walazimishwa kulipa dola thelasini za marekani.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.