Nyiragongo : Nyumba saba kuporwa na jambazi muda saa arubaini na nane pa Munigi

Nyumba saba zimeporwa na watu wenyi kumiliki silaha ndani ya Kijiji Turunga eneo la Munigi wilayani Nyiragongo, Kivu ya kaskazini.

Shirika la raia la mahali laangazia kwamba nyumba tatu ziliporwa majuzi, na kwamba zingine nne kuporwa munamo usiku wa juma tano kuamkia alhamisi tarehe 3 machi 2022. Wajambazi kupeleka vifaa kadhaa vya wakaazi.

Adolphe Shukuru prezidenti wa shirika la raia pa Munigi hujiswali kwa nini kupora nyumba siku mbili mfululizo bila kunasa majambazi.

« Tunaomba viongozi kufanya uchunguzi kwani haiwezekane kupora nyumba mbili mfululizo bila walinzi usalama kunasa watenda maovu, anena, anena prezidenti wa shirika la raia Adolphe Shukuru.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire