Kivu ya kusini : Liwali wa jimbo Théo Ngwabidje Kasi achunguza kazi za ujenzi wa barabara Industriel na Gyamba

Siku chache baada ya kuwasili mjini Bukavu, liwali wa jimbo THEO NGABIDJE KASI alitembelea nafasi kadhaa kunako fanyika ujenzi wa barabara jimboni Kivu ya kusini. Alhamisi tarehe 3 machi 2022, alijielekeza kwenyi kata Industriel na Gyamba ambako barabara zinajengwa, ili kujionea jisi kazi zaendelea kwenyi barabara Ruzizi ya pili na huko Industriel.

Katika ujumbe wa muungano wa wandishi habari toka ikulu ya liwali, Théo Ngwabidje, alianza mzunguko kwenyi barabara Industriel. Nafasi ambako shirika la kutengeneza barabara za mji OVD kwa kimombo linaendesha kazi za kutengeneza mifereji na kukarabati barabara mbele ya kuweka kabulimbu kwenyi nafasi ya mita mia tatu yenyi kuharibika.

Popote alitembelea liwali Théo Ngwabidje akizungumza na viongozi wa tabaka za chini ambao alikubali ombi lao. Hata raia walimupokea kwa furaha kuhusu kazi zinazo fanyika. Liwali wa jimbo aliahidi raia kujibu kwa swala la moto wa umeme kwenyi barabara eneo Industriel.

Kwenyi barabara Ruzizi ya pili, kazi zaendelea sambamba duru zaeleza. Huko shirika TRABMECO kwa uchunguzi wa shirika lihusikalo na kazi za barabarani Office des routes waendelea kukomesha kazi za kuachanisha barabara na wapita njia maana kazi za ujenzi wa barabara zimeboreshwa.

Ujumbe toka wandishi wa liwali waeleza kwamba raia wa Gyamba wasema kufurarishwa kuona liwali wa jimbo amerudi ili kuhitimisha kazi alizozianza, akiendelea kuziongoza na kuzichunguza binafsi.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire