Rutshuru : Mwendesha pikipiki moja ameuwawa pa Kaseguru

Mwendesha pikipiki moja ameuliwa munamo usiku wa juma tano kuamkia alhamisi tarehe 3 machi 2022 pa Kaseguru kwenyi barabara Kiwanja Ishasha, eneo la Binza wilayani Nyiragongo Kivu ya kaskazini.

Duru za mahali hunena kwamba mhanga aliuwawa alipokuwa akirudi nyumbani. Alifyatuliwa risasi kabla ya kufariki kwa majeraha.

Akihojiwa na wandishi habari, kiongozi wa eneo la Binza aomba serkali kujihusisha na usalama mdogo upande huo wa Jimbo la Kivu ya kaskazini.

 » Tunalaumu hali ya usalama mdogo inayotanda kwetu. Tunaomba viongozi kutafuta suluhu mapema« , anena kiongozi. Tufahamishe kwamba baada ya kutenda maovu, warugaruga walinyatuka na kwenda mahali pasipo julikana.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire