Bukavu : Evariste Manegabe Ntaitunda arudishwa madarakani kwenyi uongozi wa mtaa wa Ibanda

Baada ya miezi munane kusimamishwa kazi, kiongozi kwa muda wa mtaa wa Ibanda mjini Bukavu Evariste Manegabe Ntaitunda amerudishwa madarakani.

Hatua iliyochukuliwa kisheria ya barua nambari 22/022 ya tarehe 2 machi 2022 iliyo sainiwa naye liwali wa jimbo Théo Ngwabidje Kasi. Sherehe ya kubadilisha madaraka ni hii juma mosi tarehe 6 machi mwaka tunao.

Jambo hili lafurahisha mashirika kadhaa mjini Bukavu, mfano wa Fondation Maendeleo Kasha.

« Tumesikia hatua ya kurudishwa kwako kisheria madarakani, katika kibarua nambari 22/022 ya tarehe 2 machi 2022. Hii ni alama ya ujuzi wako kazini na hali ya kuishi mbele ya viongozi.

Kwa hiyo, tunakusii kutumika bega kwa bega na wafanya kazi wako, ili ya kuinua maendeleo ya mtaa wa Ibanda kwa peke na mji wa Bukavu kwa jumla. Pokea ujumbe wetu wa furaha, » kupitia ujumbe wake Wilfried Habamungu husika na mawasiliano kwenyi shirika Fondation Maendeleo Kasha.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire