Bukavu : Mwili usio na uhai wa mtoto msichana wagunduliwa kwenyi mto Ruzizi

Mwili wa mtoto mcanga usio na uhai ulikutwa ukipeperuka juu ya maji ya mto Ruzizi hii ijumaa tarehe 4 machi 2022, eneo la Kazaroho/ Ruzizi mtaani Ibanda.

Prezidenti wa shirika la raia tawi la Panzi Bwana Redouta Mweresi aliyetowa habari, anena kwamba mwili wa mtoto huyo mwenyi umri wa mwaka takriban moja na nusu uliwekwa pembeni na vijana. Hawa wakijulishwa na akina mama ambao walikuwa wakienda kwenyi soko Elakat mtaani humo Ibanda.

Shirika la raia tawi la Panzi kupitia Prezidenti huyu lalaumu tabia ya wazazi wamoja na hata walinzi wa watoto wasiojihusisha kinaganaga ndani ya uchunguzi wa watoto.

Redouta Mweresi aomba pia viongozi wa serkali kukataza akina mama wenyi kujielekeza kwenyi mto Ruzizi wakisindikizwa na watoto. Pamoja na hayo aomba kiongozi kwa muda wa kata Panzi kufanya uchunguzi ili kujuwa nini iliyopelekea kifo hicho.

Tukumbushe kwamba hadi sasa chanzo cha kifo na hata kitambulisho kwa mtoto haijulikane anena Redouta Mweresi kiongozi wa shirika la raia tawi la Panzi.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire