Mwanabunge wa taifa mcaguliwa wa Rutsburu Désiré Katembo amewasili hii juma pili tarehe 6 machi mjini Goma toka mjini mkuu Kinshasa. Kwenyi uwanja wa ndege mbele ya wandishi habari alinena kuja likizoni ili kujionea jisi hali ilivyo kabla arudi bungeni mwezi huu machi.
Huyu atoa maoni kuhusu uongozi wa kijeshi ambao umedumu kiasi bila usalama mdogo kukoma kikamilifu jimboni.
Mwanabunge Désiré Katembo akumbusha kwamba uongozi wa kijeshi ni kipindi maalum kilicho tekelezwa kisheria muda wa mwezi moja.
« Sisi kama wanabunge, tumekwisha kucunguza uongozi huo wa kijeshi mwezi agosti mjini Kinshasa, uchunguzi mwengine ulifanyika mjini Goma. Kwa kuwa tutarudi bungeni tarehe 16 machi, tutajihusisha pia na swala hilo. Tukitafuta mawazo mapya kuhusu uongozi huo ambao umedumu mno« , anena mcaguliwa wa Rutsburu.
Akikumbusha mwishowe kwamba ni miezi munane sasa tangu kutekelezwa kisheria kwa uongozi wa kijeshi mashiriki mwa DRC, yaani tangu tarehe 3 mei 2021 hadi sasa.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.