Lubero: Mtu moja kufariki dunia kutokana na kutumia mvinyo mno bila kula

Wakaazi wa Lubero

Mtu moja ameaga dunia nyumbani kwake kutokana na njaa hii juma mosi tarehe 5 machi kwenyi kata Muhangi kijiji Kikuvo, umbali kilomita kumi na mtaa wa Kirumba wilayani Lubero Kivu ya kaskazini.

Duru za mahali hunena kwamba mhanga kwa jina la Mumbere Matofali jina maarufu Shimita alikunywa pombe kiasi bila kutumia chakula na ndipo akafariki. Na kwamba alikuwa akihusika na kazi za ujenzi eneo hilo.

Bwana Salomon mtetezi wa haki ya binaadam huko, alaumu hali hiyo ya kutumia pombe za kulevya kiasi pasipo kula. Habari hii yahakikishwa na shirika la raia la Lubero.

Mazishi ya mhanga ilipangwa kufanyika kwenyi makao yake pa Kikuvo huko wilayani Lubero.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire