Kupiga marufuko kazi za kutengeneza pombe za kulevya yaani kanyanga, Mumberege, kafanya mbio, kuzidisha vikosi vya polisi pa Kasha, kuweka taa ndani ya kata zote hasa nafasi zenyi kukumbwa na giza na kadhalika.
Hizo ni moja wapo wa azimio zilizochukuliwa ndani ya kikao ili kupiganisha usalama mdogo pa Kasha mjini Bukavu. Mkutano wa watoto wa Kasha wakijumwika ndani ya shirika Fondation Maendeleo Kasha, kwa ushirikiano wa Shirika nyipya la raia NDSCI na mashirika mengine za kutetea haki ya binaadam.
Mazungumzo yalifanyika juma pili tarehe 6 machi mwaka tunao kwenyi kata Cikonyi mtaani Bagira.
Mhimizaji Wilfried Habamungu mtetezi wa haki ya binaadam pia husika na mawasiliano kwenyi shirika Fondation Maendeleo Kasha. Huyu akitowa habari, anena kwamba pamoja walizunguza kuhusu shambulizi, mauaji kwenyi eneo kadhaa za Kasha mwezi januari pa Cikonyi,Ciriri, Kanoshe, Mulwa, Mulambula, Chahi. Buholo, Kasha na hata Nyakavogo.
Kuhusu maendeleo, Wilfried Habamungu atamka kwamba mwalimu mkuu Tshangaboba alifasiria mradi kuhusu barabara ya Cikera, Mulambula, Itudu, Bwindi hadi kwenyi barabara nambari 2. Mradi ambao ulifurahisha washiriki kikao.
Akiongeza kwamba barabara zingine zenyi hali mbovu ziligusiwa na kuomba zifanyiwe utetezi mbele ya viongozi wa serkali. Pamoja na hayo wafanya siasa wenyi nia mbaya wakwamisha maendeleo ya barabara, jambo lakufwatilia kwa makini.
Duru hiyo hunena kwamba mambo mengine kadhaa yaligusiwa, yaani uwanja wa kandanda wa Kasha pamoja na mtaa wa zamani wa Kasha.
Chumba cha wandishi
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.