Nyiragongo : Wakaazi wenyi hasira wachoma mtu anayezaniwa mwizi pa Ngangi1

Shirika la raia Nyiragongo.

Mtu moja anayezaniwa mwizi alichomwa moto munamo usiku wa juma pili kuamkia juma tatu tarehe 7 machi kwenyi kijiji Ngangi ya kwanza eneo la Munigi wilayani Nyiragongo Kivu ya kaskazini.

Kutokana na Wakaaji wa mahali, mhanga alikuwa miongoni mwa wevi ambao walijaribu kuiba ndani ya nyumba kadhaa eneo hilo. Walipokimbizwa na raia, huyu moja miongoni mwao akanaswa na kupigwa, baadae kumchoma.

« Tulisikia watu wakilalamika mwizi mwizi, tulipolamuka tukakuta mtu amekata roho », aeleza akina mama moja ambaye hakupenda kutaja jina lake.

Mkaaji moja kwa jina la Alain Mukoto aomba raia kuepuka kulipisha kisasi.

« Tunaomba kutolipisha kisasi kwani ni namna ya kupoteza alama mtu akifariki « anena huyu mkaaji.

Upande wa shirika la raia la Nyiragongo, jambo hilo si nzuri kwani haijulikane kwa kweli kama wanaouliwa ndio wevi, ama ni watu wasio na hatia.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire