Goma: Akina mama moja mvunja noti afyatuliwa risasi na jambazi wenyi kushikilia silaha

Mwanamke moja mvunja noti amefyatuliwa risasi jioni ya juma tatu tarehe 7 machi 2022 na jambazi wenyi kumiliki silaha wakitembea kwa pikipiki. Ilikuwa majira ya saa kumi na moja na nusu kwenyi kiingilio TZF nyuma ya Joli hôtel katani Mapendo, mtaani Karisimbi Kivu ya kaskazini.

Duru za mahali hueleza kwamba akina mama huyo alikuwa akitoka kazini akiwa na mfuko ndogo mkononi mukiwa pesa. Majambazi hawo walimfyatuliya risasi kwenyi mkono wa kuume na kwenyi timbu, wakinyatuka na pesa.

 » Ni akina mama kwa jina la Nankavu Mapendo ndiye aligongwa risasi kwenyi mashanga njia Rutshuru majira ya saa kumi na moja na nusu. Warugaruga walinyatuka na pesa. Tunaomba msaada kwa viongozi kwani usalama mdogo unatanda mjini Goma, anena Sadiki Belo kiongozi wa kata Mapendo. Tufahamishe kwamba akina mama hakufariki hapo hapo ila alipelekwa ili ya matibabu ndani ya kituo cha afya cha mahali.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire