Kivu ya kaskazini : Mjadala wa vijana waanzishwa ili kutafuta suluhu kwa shida zao( Nathan Atibu)

Prezidenti makamu wa kwanza wa shauri la vijana nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Nathan Atibu yupo ziarani mjini Goma. Huyu akuja kushiriki kwa mjadala wa vijana jimboni Kivu ya kaskazini. Kazi zilizoanzishwa mjini Kinshasa, jimbo la Kivu ya kaskazini likichagulia la pili nchini.

Huyu aongeza kuwa wengi hujiweka ndani ya miungano mbalimbali, wakijiita kuwa watetezi wa haki ya binaadam, wengine wahusika na kazi za mazingira na kadhalika. Hiyo yapelekea serkali na washirikika kipesa kutofahamu shida kamili za vijana. » Inabidi kuorozesha vijana wa kila aina kusikiliza maoni ili kutowa mpangilio kamili kuhusu shida za vijana utakao saidia serkali na washirikika kipesa kutafuta suluhu, » anena kiongozi huyu wa vijana nchini.

« Nimeweza kuchaguliwa kama prezidenti makamu wa kwanza vijana nchini ndani ya mkutano mkuu wa nne uliofanyika pa Kisantu, ambao Prezidenti wa shauri la vijana jimboni Kivu ya kaskazini Guy Kibira aliongoza kazi. Kwa sasa ilibidi kuandaa mjadala wa vijana nchini. Kwa hiyo, kukutana na vijana, kuwasikiliza, kuchukua maoni yao na baadae kutafuta suluhu kwa shida zao, aeleza prezidenti makamu wa kwanza wa shauri la vijana nchini. Akiongeza kwamba atashariki naye kwenyi Mjadala Prezidenti wa vijana nchini binafsi.

Guy Kibira Prezidenti wa shauri la vijana jimboni Kivu ya kaskazini aliye pokea mwenziwe toka ngazi za taifa hii alhamisi tarehe 11 machi 2022, anena kufurarishwa na ujio wake Prezidenti makamu wa kwanza wa vijana nchini. Alishukuru pia juhudi za shauri la vijana nchini ambalo tayari limekutana naye Raisi wa DRC, ambaye aliahidi kuunga mkono mpango vijana toka mijadala yao.

Guy Kibira aliongoza kwamba vijana wataorozeshwa toka jimbo nzima, wanaotumika kisheria na kinyume ya sheria kwani maoni yao yahitajika ili ya ujenzi wa nchi.

Alinena mwishowe kwamba ni tayari kuacha madaraka kuhusu uchaguzi wa kamati la shauri la vijana jimboni Kivu ya kaskazini, na kwamba angali na kazi ingine ya kufanya kwa vijana na wengineo kulingana na ujuzi wake.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire