Kivu ya kaskazini : Akina mama mja mzito atekwa nyara wilayani Masisi

Masisi Rubaya

Akina mama mja mzito ametekwa nyara munamo usiku wa alhamisi kuamkia ijumaa tarehe 11 machi pa Kimoka eneo la Kamuronza wilayani Masisi.

Duru za mahali zaeleza kwamba watu wenyi kumiliki silaha wasio julikana, walijipenya kwenyi mji mdogo pa Sake nafasi iitwayo Kimoka na kupora vitu vyenyi samani, kabla ya kumteka nyara akina mama moja mzito eneo hilo.

« Uchunguzi unaendeshwa ili kujuwa mahali alipo akina mama, kwa kuwa haieleweki kuteka nyara mama aliye mja mzito. Tunaomba serkali kufanya yote iwezekanayo ili kumpata mhanga huyo. Pamoja na hayo kuhakikisha usalama kwa kuwa tunaishi na woga ndani ya eneo« , shirika la raia la mahali laeleza.

Duru zaongeza kwamba utekaji nyara wilayani Masisi ni kila leo, raia hupelekwa na watu wasio julikana, jambo linaloleta hofu kwa raia.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire