Kivu ya kaskazini/ Lubero: Wakaazi wa Kirumba na Kayna wasumbuka kwa kupanda beyi kwa nyanya (tomates)

Wakaazi wa Kirumba na Kayna wilayani Lubero wasumbuka kuhusu kupanda beyi kwa nyanya eneo hilo. Mfungo wa nyanya ambao uliuzwa franka 200 za Kongo kwa leo ni franka 400 na 500 za kongo.

Hawa wasema kwamba nyanya zilikuwa zikitokea zaidi upande wa Kibirizi. Rutshuru na Miriki pa Lubero. Wakinena kuwa usalama mdogo ni moja wapo wa ukosefu wa chakula hiyo na kupelekea kupanda kwa beyi.

Duru zetu zaongeza kwamba mbele ya nyanya kupandishwa beyi, nusu ya chakula hiyo ilikuwa ikitokea huko Graben ambako walimaji walifukuzwa na walinzi wa mbuga la kuhifadhi wanyama la Virunga. Na kwamba ni kiasi ndogo ya nyanya ndio yapatikana kwa sasa pa Kayna na Kirumba.

Alipoulizwa kuhusu kukomesha hali hiyo ya ukosefu wa nyanya maoneo hayo, Kasereka Mutahinga moja wa ma wataalam wa kilimo pa Lubero anena kuwa inabidi walimaji wapate shauri toka wataalam wa kilimo, pia waweze kulima wakiheshimu desturi katika kulima nyanya.

Mtaalam huyo anena kuwa eneo nyingi za Béni ambazo zilikuwa zikitowa nyanya zakumbwa kwa usalama mdogo. Akiongeza kwamba nafasi nyingi Butembo hazina mboleo, miti imelimwa nafasi kadhaa pa Lubero ambayo yaharibu udongo.

Kuhusu kupanda beyi kwa nyanya, mtaalam Kasereka Mutahinga anena kwamba inabidi mazao ya nyanya yalinganishwe na ombi la wakaazi, hapo hali itabadilika.

Issa Lubiri

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire