Masisi: Msichana mwenyi umri wa miaka kumi na saba atekwa nyara

Majambazi wenyi kumiliki silaha waliteka nyara msichana mwenyi umri wa miaka kumi na saba munamo usiku wa juma mosi kuamkia juma pili tarehe 13 machi 2022. Hayo yalifanyika katika kitongoji cha Nyamitaba mkoani Bashali Kayembe.

Duru toka huko zanena kwamba mhanga alishikwa nyumbani kwao na kupelewa mahali pasipo julikana.

Shirika nyipya la raia la mahali lanena kwamba walinzi wa usalama walijaribu kuokowa mhanga, wakifyatuwa risasi ila hawakufaulu.

Shirika hilo la kufetea haki za binaadam likipasha habari kwa media mjini Goma, laomba vyombo vya usalama kuzidisha nguvu katika uchunguzi hadi vitakapo mpata mhanga mahali alipo, akiiwa kwa jina la Rachel.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire