
Kuonyesha matendo yenyi kuchochea amani pamoja na kuunda kamati ya ufwatiliaji wa hatua zilizochukuliwa. Ni miongoni mwa hatua zilizochukuliwa wakati wa mazungumzo muda wa siku mbili ikikutanisha viongozi wa wilaya ya Masisi.
Prezidenti makamu wa kwanza wa muungano wa makabila Kambale Siriwayo anena kwamba watoto wa Masisi waliongea jicho kwa jicho, na kwamba waliambiana ukweli. Pamoja na hayo kutupilia mbali tabia ya unafiki kama ilivyo mbeleni, katika lengo la kutekeleza amani.
Upande wa serkali, kikao hicho ni mhimu ajili ya ujenzi wa amani wilayani Masisi, ambayo ni gala ya nchi ya Zaïre ya zamani. Serkali iliahidia kusindikiza kazi hizo ili kufikia lengo, yaani amani ya kudumu eneo hilo jimboni Kivu ya kaskazini. Pamoja na hayo kutapanya habari kwa mashirika za usalama na kuhamasisha raia kuhusu matokeo ya kikao. Na kuomba vijana kuingia jeshi ili kulinda usalama makwao.
Tufahamishe kwamba kuliundwa kamati ya ufwatiliyaji wa matokeo ya kikao itakayo husika na maeneo zenyi mizozo hasa.
Chumba cha wandishi
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.