Goma: Mtoto Joas apatikana baada ya kutekwa nyara na jirani yake

Prezidenti wa shauri la vijana mtaani Karisimbi afurahi na kujihusisha kwa vyombo vya usalama, kwa kumpata mtoto Joas aliyetekwa nyara juma lililopita pa Ndosho.

Prezidenti huyu kwa jina la Claude Rugo anena kuwa ni jirani ya jamaa ya mtoto ndiye aliweza mteka nyara na kumpeleka huko Rubaya wilayani Masisi.

Huyu anaomba vyombo vya usalama kuzidisha nguvu ili kugunduwa visa vingine vya wahanga wa utekaji nyara jimboni Kivu ya kaskazini.

« Tunayo machozi ya furaha kuhusu kumpata mtoto Joas kwa vyombo vya usalama ambaye duru zanena kwamba ni jirani ya mtoto ndiye aliweza mteka nyara. Tunahitaji jirani huyu mtenda maovu apelekwe mbele ya sheria na ahukumie kwa makosa yake« , anena Prezidenti wa shauri la vijana mtaani Karisimbi.

Tufahamishe kwamba ni tangu zamani visa vya utekaji nyara vyaripotiwa kila leo kote jimboni Kivu ya kaskazini.

Issa Lubiri

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire