Kivu ya kaskazini : Raia wenyi kuishi kando ya mbuga la Wanyama la Virunga wapinga kuongeza udongo kwa eneo la shamba hilo

Watu wenyi kuishi kando ya mbuga la kuhifadhi wanyama la Virunga magaribi mwa ziwa Édouard kusini mwa mtaa wa Lubero waliandamana majuzi.

Duru za mahali zanena kwamba ni namna ya kupinga mbuga la kuhifadhi wanyama kuongeza eneo lake kwa kuchukuwa vijijini vya Mirimba. Tariha na Kisirira.

Duru zaangazia kwamba waandamanaji walitokea Taliha hadi Ntwali mahali ambako walipeleka kibarua cha malalamiko yao kwenyi shirika ICCN.

Mkaaji moja aangazia la ronde info kwamba katika kibarua chao raia waomba shirika ICCN kurudisha udongo huo ama kuacha njama kupitia kuongeza udongo kimagendo.

Kwa hiyo, kiongozi wa wilaya ya Lubero aliomba raia kubaki tulivu. Mkaazi huyu akihojiwa kuhusu mazungumzo inayoandaliwa ajili ya shamba la wanyama la Virunga , alinena kwamba mazungumzo hayo ni kwa manufaa ya walinzi peke, na kwamba maandamano ni haki yao.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire