Kivu ya kaskazini : Vijana wa Véranda Mutsanga waahidia kusindikiza wanafunzi kupinga kupandishwa kwa pesa za kushiriki mtihani wa serkali Patient Rafiki akiangazia kuwa pesa hazikupandishwa

Kivu ya kaskazini.

Vijana wa Muungano Véranda Mutsanga wasema kwamba wataunga mkono wanafunzi wa shule la sita la sekondari kuhusu kupandishwa kwa pesa ili kushiriki kwenyi mtihani wa serkali.

Katika ujumbe wao, vijana hawo wanapinga kibarua alicho kisaini kisheria liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini Constant Ndima Kogba.

Vijana wa Véranda Mutsanga wanena kwamba ni mshangao kuona viongozi wa kijeshi hawana huruma kwa raia. Ijapo wafahamu usalama mdogo na hali mbovu kiuchumi ya raia.

Patrick Ricky Paluku anayesaini ujumbe anena kwamba ni akina mama kwa leo ndio wahudumia jamaa, kwa kuwa waume wakosa kazi. Pamoja na hayo raia hawafike shambani wakihofia maisha. Muungano huwo wasema kwamba ingelikuwa heri jimbo la Kivu ya kaskazini lihudumiwe kipekee kulingana na shida linalopitia.

Upande mwengine Patient Rafiki kiongozi mwenyi kutetea haki za walimu wa shule la kiprotestanti alitowa mwanga kuhusu pesa hizo, akionyesha kwamba hazikuonzeka. Huyu afasiria kuwa pesa hazikupandishwa ila zilitajwa zote kwa jumla 121000fc hadi kuogopesha wazazi. Kinyume na hapo mbeleni wakati serkali ilikuwa ikitaja moja kwa moja pesa zenyi zitalipwa na kufikia hizo hizo zimeombwa kwa leo. Patient Rafiki aongeza kuwa pesa hizo zitalipwa vipande kwa vipande hadi kukomesha.

Issa Lubiri

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire