Lubero : Kiongozi wa Kyambene mtaa wa asili wa Kirumba afariki dunia kwa kujitundika

Kiongozi wa eneo Kyambene katani Makasi mtaa wa asili wa Kirumba alifariki dunia kwa kujitundika. Hayo yalifanyika munamo usiku wa juma nne kuamkia juma tano tarehe 16 machi 2022 nyumbani kwake.

Duru za mahali zaeleza kwamba mhanga alijitundika kutokana na shida zilizo mkumba nyumbani kwake

 » Tulimkuta asubui ya juma tano tarehe 16 machi, kiongozi huyo akiwa na kamba shingoni, akiwa na kikartasi ambacho kunaangazia kama amejiondolea maisha kutokana na shida alizo nazo nyumbani kwake » mkaazi moja anena.

Tujulishe kwamba mhanga ameacha mjane na yatima saba.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire