Kivu ya kusini : Makanisa zaunga mkono liwali wa jimbo Théo Ngwabidje Kasi ili aendeshe vema miradi ya maendeleo

Mji wa Bukavu Kivu ya kusini

Habari toka chumba cha mawasiliano cha liwali wa jimbo zaeleza kwamba baada ya ujumbe wa arkiaskofu François Xavier Maroy kuhusu umoja na kuungana mkono, ni muda wa kanisa za Kristu nchini DRC ECC kwa kimombo, za uamsho na za waislamu kujitokeza.

Kanisa hizo zaomba raia jimboni Kivu ya kusini kukomesha mizozo, na kusitiza umoja, amani na ushirikiano kijamii. Hayo hupelekea maendeleo ya jimbo kama ilivyo matakwa yake liwali wa jimbo Théo Ngwabidje Kasi mwenyewe.

Viongozi wa makanisa walinena hayo ijumaa tarehe 18 machi mbele ya liwali, wakisisitiza kuhusu ujenzi wa jimbo na maendeleo. Liwali alikutana moja kwa moja na viongozi wa makanisa kadhaa yaani prezidenti wa ECC, 5ème CELPA, waislamu ambao waliomba kuacha liwali aweze kutekeleza miradi ajili ya maendeleo ya jimbo.

Duru hiyo yaeleza kwamba ilikuwa fursa kwake liwali kupokea baraka na shauri toka watumishi wa Mungu ili afaulu kujibu kwa shida za raia. Mkutano huo siyo ya kwanza kwani aliwahi kutanana na viongozi wa kijamii na kisiasa ili ya ujenzi wa jimbo ambayo ni matakwa yake Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire