RDC : Patrick Katengo Mafo aalika vijana kujihusisha kwa kupiganisha mabadiliko ya mazingira

Ajili ya siku kuu ulimwenguni ya kuinua mazingira, Prezidenti wa muungano wa vijana nchini DRC kwa maarufu balozi wa amani Patrick Katengo Mafo atoa ujumbe mhimu kuhusu maisha kwa raia ulimwenguni kwa jumla na nchini DRC kwa peke.

 » Ulimwengu unaishi katika hatari kubwa kuhusu kuharibu mazingira na mambo mengine inayoichafuwa. Tukifunga mikono watakao ishi nyuma yetu watateswa vikali kupita sisi, » anena Kiongozi huyu wa vijana.

Yeye aomba vijana kujihusisha kuboresha mazingira kupitia miradi mhimu ya kutengeneza vitu vipya. Patrick Katengo aomba kuwa na zamiri ili kupunguza maafa ya mazingira kutokana na matumizi mabaya.

Akijibu kwa maswali ya wandishi habari huyu aomba serkali na mashirika kadhaa kuunga mkono miradi ya vijana kuhusu ulinzi wa mazingira.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire