Maji safi ni shida kubwa katika vijiji yapata ishirini na nane wilayani Nyiragongo jimboni Kivu ya kaskazini.
Alifahamisha hayo kwenyi vyombo vya habari vimoja vya mahali Bwana Bosenibamwe Muzungu kiongozi wa shirika la kutetea haki za binaadam ACADEPA ZABURI 133. Alihakikisha hayo hii juma nne tarehe 22 machi 2022 ajili ya siku kuu ulimwenguni ya maji safi.
Duru zingine hunena kwamba raia kadhaa wa vijijini hivyo hufunga safari ili kutafuta nafasi ambako maji hayo yaweza patikana, jambo lenyi kusababisha vinyume yaani ajali za barabarani, hatari ya kubakwa kwa wasichana na kadhalika.
Kumbukeni kwamba uhaba wa maji safi wasababisha maradhi kutokana na mikono michafu yaani kipindupindu na kadhalika.
Issa Lubiri.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.