Goma: Wanabunge wa taifa Hubert Furuguta pamoja naye Patrick Munyomo wafurahishwa na kazi za ujenzi wa barabara Kilijiwe

Wanabunge wa taifa Hubert Furuguta pamoja naye Patrick Munyomo wametembelea hii juma tano tarehe 23 machi kwenyi barabara Kilijiwe ili kujionea binafsi jisi kazi zaendeshwa eneo hilo. Ni mita 1/2 ndio imejengwa dhidi ya 3/7. Wakijibu kwa maswali ya wandishi habari, hawa walinena kufurarishwa na namna kazi za ujenzi wa barabara hiyo zaendeshwa.

Wanabunge hawo walisema kwamba kazi hizo ni matokeo ya utetezi waliofanya mbele ya viongozi wa serkali mjini Kinshasa hususan mbele ya Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO.

« Tulifika hapa ili kufwatilia gisi kazi zinaendelea, mbele tuligundua hitaji ya raia, pia tukafanya utetezi kama wabunge wa taifa, serkali kuanza kazi na washirika wake kuisapoti na sasa ni muda wa kufwatilia gisi kazi zaendeshwa, anena mwanabunge mchaguliwa wa Goma Hubert Furuguta.

Upande wake mwanabunge Patrick Munyomo , waziri wa mambo ya ujenzi amefanya vema ambaye alijibu kwa ombi lao yeye na mwenzake Hubert Furuguta ambao walikwenda kumuona pamoja, na kwa leo ana furaha kubwa kuona kazi zimeanza kutekelezwa.

Niliwahi kupita hapa siku moja na kujiswali tuko Goma ama la. Naunga mkono washirika wa serkali yaani umoja wa ulaya kwa kusapoti kazi anena mwanabunge Patrick Munyomo

.

Raia tuliowakuta mahali hapo walinena kwamba ujenzi wa barabara hiyo imekawia mno, na wanaamini kwamba ni muda wa kuhitimisha kazi za barabara wakiwaona wanabunge mahali hapo.

Tufahamishe kwamba barabara hiyo yenyi samani kubwa mjini ni yenyi hali mbovu mno kunako kata Majengo hasa, ambako gari, pikipiki na hata wapita njia wasongamana kutokana na maji na hata matope yenyi kujaa nafasi hiyo.

Juvénal Murhula.

« 

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire