Masisi : Raia waendelea kuwa wahanga wa utekaji nyara

Watu tatu waliteka nyara juma nne majuzi na watu wenyi kumiliki silaha wasiojulikana. Hayo yalifanyika kwenyi barabara Kitsanga Nyakabingu nafasi iitwayo Rugarama, eneo la Bashali Mokoto.

Duru za mahali zaeleza kwamba mwendesha pikipiki moja aliyekuwa akisafiri na wateja wawili mjini Goma ndiye alitekwa nyara na jambazi wenyi kushikiliya silaha, ambao walipeleka msituni.

« Tunaomba serkali kulinda usalama wa raia pa Masisi ambako visa vya mauaji na utekaji nyara ni chungu tele« , laeleza shirika la raia la mahali.

Tufahamishe kwamba hakuna ripoti kuhusu kuachiliwa kwa wahanga wa utekaji nyara hao tangu majuzi.

Issa Lubiri

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire