Maniema : uchaguzi wa liwali jimboni humo ni hapa karibuni

Liwali kwa muda jimboni Maniema.

Akiwasili kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma hii juma nne tarehe 29 machi, liwali kwa muda jimboni Maniema Alfani Idrissa anena kuja mjini Goma ili kuzungumza na wanamemba wa chama UDPS Kivu ya kaskazini.

Akihojiwa kuhusu uchaguzi wa liwali hapa karibuni jimboni humo, alinena kwamba yupo kandideti kwenyi uchaguzi huo. Akiahidi kubuga ushindi kupitia chama chake UDPS kinacho lenga maendeleo na kijamii.

« Kupitia Muungano Union sacrée, nilichaguliwa mimi mtumishi wenu Alfani Idrissa kama kandideti upande wa muungano huo. Hakuna muungano Union sacrée bila chama UDPS. Nafasi chama hicho kilicho, ni nani ataweza kushinda muungano Union sacrée, »anena kwa muda jimboni Maniema.

Huyu aomba makada wa chama chake kuunga mkono katibu mkuu wao Augustin Kabuya, dhidi ya machochezi kuhusu mgawanyiko wa muungano Union sacrée. Baadae atajielekeza huko Maniema jimboni mwake.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire