Mwakilishi wa chama UNC chake Vital Kamerhe jimboni Kivu ya kusini, Daniel Lwaboshi aendesha kazi za maendeleo wilayani Kabare. Ni tangu wiki iliyopita akisindikizwa naye Pasta Tonde Kaheto.
Duru zetu zanena kwamba hawa wameanza karabati vilalo vya Cikumbo na nafasi iitwayo kwa Kamole eneo la Luhihi. Ni katika lengo la kurahisisha mawasiliano kati ya kituo cha afya cha Izimero na hospitali ya Fomulac pa Katana.
Daniel Lwaboshi pamoja Pasta Tonde Kaheto walitambua shida za wagonjwa ndani ya kituo cha afya Daktari Assani Bashwira huko Mugererebo pamoja na zile za akina mama wenyi kujielekeza kwa vipimo.
Wote wawili walitowa mabati kumi na miti thelasini kwa kituo cha afya majuzi mbele ya raia walio wengi, waliofurahishwa na kitendo hicho.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.