Goma : Nyumba nyingi zimeporwa ndani ya kata zaidi tatu

Nyumba nyingi ndani ya kata kadhaa mjini Goma zimeporwa na watu wenyi kumiliki silaha wasiojulikana usiku wa juma mosi kuamkia juma pili tarehe 3 aprili 2022.

Kutokana na duru zetu, ni kata Katoyi, Ndosho, Bujovu, Kyeshero. Murara, Mugunga na kadhalika ndizo ziliweza kushambuliwa .Vitu vyenyi samani kubwa viliporwa ndani ya nyumba za kata hizo.

Raia wa mahali waomba viongozi wa kijeshi kurejesha hali ya usalama mjini Goma kwa peke na jimboni Kivu ya kaskazini kwa jumla.

« Kweli tuna huzuni kuona zaidi ya nyumba saba kuporwa ndani ya kata Ndosho upande wa station Simba bila walinzi wa usalama kujitokeza. Tulijaribu kuita nambari ya kimanjani pasipo kufaulu, » wakaazi waeleza.

Duru zingine hunena kwamba hayo yatokana na idadi ndogo ya askari polisi pamoja na ukosefu wa vifaa vya kazi

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire