Goma : Ajali ya barabarani saa za jioni huko Katindo2 mtaani Karisimbi.

Ajali ya barabarani ilifanyika hii juma nne tarehe 5 aprili 2022 majira ya saa kumi na mbili na nusu pa Katoyi mtaani Karisimbi .

Baba moja mwenyi umri wa miaka kati ya hamsini na sitini aligongwa na mwendesha pikipiki ambaye alikuwa akitembeza kwa mwendo wa kasi.

Hayo yalifanyika kwenyi barabara Kilijiwe entrée du Président wakati mhanga alijaribu kuvuka akitokea upande wa soko ya Katindo2.

Mwendesha pikipiki ambaye hakujulikana baada ya kugongwa kwa mhanga alinyatuka na kwenda zake. Hapo hapo watu wenyi moyo mwema miongoni vijana walimpeleka kwenyi kituo cha afya cha karibu.

Tufahamishe kwamba hakuna kiongozi hata moja wa mahali alikuweko muda wa dakika thelasini tangu alipogongwa mtu huyo.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire