Goma : Mtu moja ajeruhiwa kwa risasi na watu wenyi kushikiliya silaha

Mtu moja alijeruhiwa kwa risasi kwenyi kata Katoyi na watu wenyi kumiliki silaha wasiojulikana. Hayo yalifanyika asubui ya juma pili tarehe 3 aprili 2022 eneo za shule École de l’unité.

Prezidenti wa vijana pa Katoyi Prince Baninge anena kwamba mhanga ni Innocent Cirimwami ambaye alikwenda kutafuta kuni ya kuwasha moto mahali pa kilio .

 » Bwana Innocent Cirimwami alikwenda kutafuta kuni ili kuwasha moto mahali pa kilio. Ndipo kuanguka ndani ya nyavu za majambazi wanne wenyi kushikiliya silaha ambao kumujeruhi kwa kumufyatuliya risasi, anena Prezidenti wa vijana pa Katoyi« . Akiongeza kwamba ni watu tano ndio waliokwenda kusaka kuni ili kuwasha moto mahali hapo

Prince Baninge aomba viongozi kuwalindia usalama kwani hali yaendelea kuzorota kila leo mjini .

Tufahamishe kwamba mhanga alipelekwa kwenyi kituo cha afya Caritas kabla apelekwe kwenyi hospitali ya CEBCA pa ndosho kutokana na kuvunjika kwa mguu.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire