Goma : François Nzekuye akuja kupongeza wahanga wa vita wilayani Rutshuru

Ninaomba raia wa wilaya ya Rutshuru kuunga mkono jeshi la taifa ili ya kupiganisha adui. Nawaahidi kwamba niko nikijihusisha na shida inayowakumba ili wapewe msaada toka serkali. Pamoja na hayo nawapa pôle.

Matamshi yake mwanabunge wa taifa François Nzekuye alipowasili kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma toka mji mkuu Kinshasa.

Mwanabunge huyo mchaguliwa wa Rutshuru anena kwamba atarudi haraka mjini Kinshasa ili kushiriki katika kikao bungeni ambamo watazungumzia mambo ya siasa peke.

François Nzekuye ana mashaka kuhusu uchaguzi unaoandaliwa mwaka 2023, kwa kuwa watakao andaa uchaguzi huo kwenyi tume huru ya uchaguzi Ceni ni wanamemba pia wa chama UDPS. Mwanabunge huyu ana mashaka hata kuhusu wanamemba wa korti kuu ya katiba ambayo ina mamlaka ya kuhakikisha matokeo ya uchaguzi.

Mwanabunge asisitiza kwamba inabidi swala hizo na zingine ziweze kutatuliwa ndani ya kikao bungeni mbele kufikia uchaguzi ujao.

Kabla ya hapo, alijielekeza kwenyi ofisi ya chama chake mjini Goma ambako alihotubia wanamemba wao kuhusu hali ya kisiasa kwa sasa.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire