Goma : Placide Kambere Nzilamba aomba Raisi wa DRC kuwa makini kwa kutowaingiza jeshini ama serkalini waasi wa M23

Katibu hausika na mambo ya ufundi kwenyi shirika la raia Kivu ya kaskazini Placide Nzilamba aomba Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI kuwa macho, kuhusu swala la waasi wa M23.

Huyu azani kwamba kufanya majadiliano na waasi hawo ni namna ya kuvunja nguvu za nchi, katika lengo la kurejesha amani nchini humo.

Nzilamba asisitiza kwamba kuingiza waasi hawo ndani ya jeshi ama kwenyi uongozi wa nchi haiwezi leta suluhu kwa swala la usalama mdogo mashariki mwa DRC.

« ‘Watu wameuwawa , wameporwa mali na hata kuyahama maskani yao. Wanamugambo M23 hawana bahati ya kupewa uongozi kutokana na mwenendo wao mubaya. Na ndio maana tuko naomba Raisi wa DRC asiingie katika lengo lile. Kama wakitaka kurudi waanze kama makundi mengine. Waingie ndani ya mpango PDDRCS , wajisalimishe,

Kiongozi huyu afasiria kwamba wakiingia ndani ya jeshi na ndani ya serkalii ni kama Raisi amesema mpango PDDRCS uvunjike, anena katibu hausika na mambo ufundi kwenyi shirika la raia Kivu ya kaskazini.

Nzilamba asema kwamba ndio maana hawata kubali mambo kama na hayo.

Tunaomba raia waanze kujitayarisha kufanya matendo ya kukataa hawo wanamugambo wa M23 waingie ndani ya jeshi ama serkalini, akomesha matamshi yake Jacques Nzilamba.

Issa Lubiri.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire