Watekaji nyara waliomteka mtoto moja mwenyi umri wa miaka munane kwenyi kata Mugunga walazimisha dola 1500 za marekani ili aachiliwe huru mtoto.
Duru zenyi kuaminika zaeleza kwamba mtoto alitekwa nyara tangu juma tatu na tangu juma nne saa za mchana ndipo wanyanyasi hawo walianza kulazimisha kiwango hicho cha pesa, na kama sivyo mtoto auwawe.
» Watumishi wa shirika la mawasiliano Airtel, hawawezi kugunduwa mahali watenda maovu hawo wafichama, kwa kuwa watumia namba ya shirika hilo la mawasiliano. Tunaomba raia kuwasiliana vilivyo na vyombo vya usalama ili kugunduwa jambazi hawo. Pamoja na hayo, serkali kuweka mkazo kuhusu usalama mjini Goma hususan katika kata Mugunga, » anena Prezidenti wa shirika la raia katani humo.
Tujulishe kwamba baba wa mtoto aliye tekwa nyara anena hana msaada wowote ule ili kumtowa mwanawe mikononi mwa watekaji nyara, akitumaini nguvu za serkali.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.