
Mtu moja kutekwa nyara na watu wasiojulikana jioni ya juma mosi tarehe 2 aprili 2022 ndani ya kijiji Muheto eneo la Kayembe jimboni Kivu ya kaskazini.
Duru toka huko hunena kwamba mtu huyo kwa jina la Saidi Nzaho alitekwa nyara tangu juma mosi alipokuwa akitokea kazini. Watekaji nyara wasisitiza wapewe dola 1000 za marekani ili aachiliwe.
Vijana wa kijiji Muheto waomba viongozi wa serkali kujihusisha katika swala hilo, ili aweze kupatikana mhanga. Wadadisi wa mambo waendelea kujiswali, mkulima atowe dola 1000 za marekani wapi kwa rafla ili aachiliwe?
Issa Lubiri.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.