
Waziri wa mazingira pia utalii yupo jimboni Kivu ya kaskazini ili kuchunguza jisi kazi zaendeshwa ndani ya sekta yake yaani mazingira na utalii.
Modero Nsimba Matondo anena hayo alipowasili kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, hii alhamisi tarehe 7 aprili 2022.
« Namna mbuga la kuhifadhi wanyama la Virunga linachungwa, kuzungumza kuhusu miradi mbalimbali kuhusu shamba hilo, namna raia wafaidia miradi hiyo na kadhalika, »anena waziri wa taifa Modero Nsimba.
Huyu aongeza kwamba atakutana pia na viongozi wa mbuga la kuhifadhi wanyama la Kahuzi Biega, ili kupata mwanga kuhusu vitendo vya ujeuri wanavyo shutumiwa walinzi wa shamba la wanyama hilo.
Akihojiwa kuhusu hali ya usalama mdogo kwenyi mbuga la wanyama la Virunga, waziri alitamka kwamba jambo hilo ni lake waziri husika na ulinzi pamoja na liwali mwanajeshi. Akisisitiza kwamba atakutana na wanamemba wa shauri la uongozi wa mbuga la wanyama.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.