Bukavu : Shirika ndogo la raia katani Panzi laomba uongozi wa eneo hilo ubadilishwe kwani ni miaka mingi bila maendeleo

Kata Panzi

Katika matamshi yake kwenyi Mama Redio mjini Bukavu, prezidenti wa shirika ndogo la raia katani Panzi Redouta Mweresi Aruta aomba uongozi wa kata hiyo kubadilishwa. Uongozi umedumu miaka karibu ishirini bila mabadiliko yoyote ile.

Mwalimu huyu pia mtetezi wa haki ya binaadam ataja mfano wa kiongozi wa kitongoji moja ya Panzi ambaye alichukuwa hatua ya kubomowa vyoo vya shule la msinji du Lac la huko, bila woga wowote ule.

Kwa hiyo, shirika ndogo la raia la Panzi kupitia Redouta Mweresi laomba kiongozi wa mtaa wa Ibanda kubadilisha mapema uongozi huo , ambao umekwamisha maendeleo ya huko miaka chungu tele. Na kama sivyo, shirika hilo laahidi kufanya maandamano kwenyi ofisi ya kiongozi wa mtaa.

Wakati wa mwaliko huo tedioni aligusia swala la wizi unaoendeshwa na watoto wa mitaani , walifukuzwa pa Essence na kujielekeza ndani ya vitongoji vya kata, wakifanya operesheni zao.

Pamoja na hayo ajali za barabarani kutokana ukosefu wa barabara za kando, wenyeji gari na pikipiki wakitumia barabara moja peke. Huyu aomba serkali kutafuta suluhu kwa swala.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire