Goma: Tony Mwaba akutana na viongozi wa sekta ya elimu jimboni Kivu ya kaskazini na kusini ili kutafuta suluhu kwa shida ndani ya sekta hiyo

Ninatoka kukutana na viongozi wa sekta ya elimu jimboni Kivu ya kaskazini na kusini kama kawaida. Pamoja tukizungumzia shida zenyi kukumba sekta hiyo. Kwa sasa naona gisi hali ilivyo. Naalika kila majimbo kufanya kazi mahali zlipo, na sisi tutafanya kazi inayotuhusu mjini Kinshasa.

Matamshi yake waziri husika na elimu ya msinji, sekondari pia kiufundi Tony Mwaba baada ya kukutana na viongozi wa sekta ya elimu wa majimbo hayo mawili.

Tony Mwaba aambia waandishi kwamba ilibidi kujuwa shida za peke kwa kila jimbo, ila kwa jumla majimbo yaonekana kuwa na shida zimoja yaani kuwalipa walimu wapya, kulipa kupitia benki, aina gani ya mafunzo na kadhalika.

Kwa hiyo, iliombwa kila moja mahali alipo kufanya kazi ili kuboresha sekta ya elimu nchini anena waziri husika na elimu ya msinji, sekondari pia kiufundi.

Tufahamishe kwamba waziri atatembelea majimbo za Kasaï siku za usoni kuhusu kazi hiyo.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire