Kivu ya kaskazini : Jeannette Mapera aendesha utetezi kutokana na usalama mdogo jimboni humo

Mwanabunge wa taifa Jeannette Mapera yuko tangu juma pili tarehe 10 aprili mjini Goma ili kutayarisha ujio wake waziri mkuu Sama Lukonde. Ambaye akuja kucunguza binafsi matokeo ya uongozi wa kijeshi jimboni Kivu ya kaskazini na Ituri. Huku malalamiko yakitokea hapa na pale kuhusu uongozi mbovu ya uongozi huo.

Akihojiwa na wandishi habari kuhusu uongozi wa kijeshi jimboni, Mapera aonyesha hali ilioko siku hizi pa Rutshuru, mapigano kati ya jeshi la taifa na waasi wa M23. Na kwamba hayo yote ndio sababu ya kuja kwake waziri mkuu, ambaye mbele ya yote kuwapongeza askari jeshi wenyi kupambana na waasi.

« Pamoja na hayo, waziri mkuu atakutana na wanachuo, makanisa, miungano ya shirika la raia kwa jumla ili kutowa maoni kuhusu uongozi wa kijeshi na hata nyingi wandishi habari, mambo munayoyaishi kila leo« , anena mwanabunge mchaguliwa wa Lubero, akikumbusha kwamba uongozi wa kijeshi unatoka kuongezewa mhula wa mara 21 hapa majuzi.

Tukumbushe kwamba baada ya Kivu ya kaskazini, waziri mkuu atajielekeza pa Ituri kabla ya kurudi mjini Kinshasa.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire