Goma : Moto wa umeme wateketeza nyumba munane Mabanga ya kusini

Ofisi ya mtaa wa Goma.

Nyumba munane zimewaka moto kwenyi kata Mabanga ya kusini kitongoji cha Kisimba mtaani Goma Kivu ya kaskazini.

Duru za mahali zaeleza kwamba moto ulianza ndani ya nyumba moja yenyi kuhudumiwa na shirika SNEL, ukiambukia nyumba zingine, na watu kupoteza vitu vyenyi samani kubwa.

Tulikuwa wahanga wa ajali ya moto saa za usiku. Mungu amesaidia kwani hakuna mtu aliyefariki dunia. Tunaomba msaada kwa mtu yeyote wa moyo mwema, anena Kyakimwa Ange moja wa wahanga wa ajali hiyo ya moto.

Kiongozi wa kata Mabanga ya kusini aomba wakaaji kutowa msaada kwa wahanga, ambao wamepoteza vitu na hata kulala nje.

Issa Lubiri

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire