Kivu ya kaskazini : Pamoja na mcango wa raia waaziri mkuu Sama Lukonde aahidi suluhu kwa shida zao

Waziri mkuu Jean Michel Sama Lukonde

Ni dola milioni 33 za marekani mwanzoni zilizotumwa kwa mikono ya jeshi la taifa, pesa zingine zitafwata ili kujibu kwa swala la usalama mdogo mashariki mwa DRC.

Ni matamshi yake waziri mkuu wa DRC Sama Lukonde wakati wa mkutano na waandishi habari kabla ya kuhitimisha ziara ya kazi jimboni Kivu ya kaskazini na kujielekeza jimboni Ituri.

Waziri mkuu alitembelea nafasi kadhaa jimboni yaani uwanja wa ndege pa Mugunga, wahanga wa moto wa volkeno pa Nyiragongo, uwanja wa ndege wa Goma, barabara na kadhalika katika lengo la kucunguza kazi za maendeleo. Pamoja na hayo kuzungumza na miungano ya shirika la raia na hata viongozi wa serkali, ili kucunguza pamoja mwenendo wa uongozi wa kijeshi na swala la maendeleo.

Baadae akijibu kwa maswali ya wandishi habari, kujuwa kama mazungumzo yatakueko kati ya serkali na waasi wa M23, kuwaazibu wale wote wanaosabisha rushwa wakila pesa za jeshi, kujibu kwa maswala za ndani kiutu na kiopresheni. swala la uongozi wa asili wa Bukumu, kuomba wajiepushe wote wanaounga mkono waasi, swala la uchaguzi na kadhalika.

Kwa mambo hayo yote waziri alitamka kwamba serkali ya nchi itajitahidi kuleta suluhu moja kwa moja ili kutekeleza amani ya kudumu.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire